Header Ads

CHADEMA wafuta mikutano ya hadhara, kuungana na Taifa kupambana na virusi vya Corona

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kupitia kwa Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, kimetangaza kusitisha kufanya mikutano yake ya hadhara nchi nzima, kama kilivyokuwa kimetangaza na badala yake kitaungana na Taifa katika kupambana na janga la ugonjwa wa Virusi vya Corona.
Image result for freeman mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Akizungumza leo Machi 23, 2020, Jijini Dodoma, Mbowe amesema kuwa wakati anatoa kauli yake ya kutangaza uwepo wa mikutano ya hadhara kwa nchi nzima, Serikali haikuwa imetangaza uwepo wa mgonjwa yeyote wa Virusi vya Corona na kwamba wataendelea na mikutano yao pale ambapo hali ya ugonjwa huo itakuwa imetengemaa.
“Na moja ya ushauri uliotolewa ni pamoja na kuzuia mikusanyiko mikubwa mikubwa, kwahiyo sisi tutaahirisha shughuli zote hizo za mikusanyiko mikubwa ndani ya chama chetu na tutashirikiana na Watanzania wenzetu kuchukua tahadhari ili kuhakikisha kwamba tunaweza kupambana kikamilifu na janga hili la Corona” amesema Mbowe.
Aidha Mbowe ameiomba Serikali ione ipo haja ya kufunga mipaka yake yote ili kuhakikisha hakuna mgeni yoyote anayeingia nchini kutoka kwenye Mataifa yaliyoathirika na Virusi vya Corona.

No comments:

'; (function() { var dsq = document.createElement('script'); dsq.type = 'text/javascript'; dsq.async = true; dsq.src = '//' + disqus_shortname + '.disqus.com/embed.js'; (document.getElementsByTagName('head')[0] || document.getElementsByTagName('body')[0]).appendChild(dsq); })();

Popular Posts